GENEVA: DDT kutumiwa tena kupiga vita malaria
16 Septemba 2006Matangazo
Shirika la Afya Duniani-WHO limetoa wito kwa nchi zinazoendelea hasa barani Afrika kuanza kutumia dawa ya DDT ndani ya nyumba kupiga vita malaria.Dawa ya DDT tangu muda mrefu imepigwa marufuku Marekani na nchi nyingi zingine kwa sababu ya madhara ya mazingira,yanayoweza kusababishwa na dawa hiyo ya utata.Lakini mkurugenzi wa WHO,Dr.Arata Kochi amesema,DDT inasaidia kupambana na malaria na kwamba dawa hiyo haina hatari ikipigwa ndani ya nyumba. Malaria ni ugonjwa unaoua kama watu milioni moja kila mwaka-wengi wao wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.