Gaza. Wapalestina waandamana kupinga wayahudi kuingia katika maeneo nyeti ya Jerusalem.
9 Aprili 2005Zaidi ya Wapalestina 10,000 wameandamana leo na kuonya kuwa kutakokea machafuko kwa mara ya tatu iwapo Wayahudi wenye imani kali ambao wanatarajia kuharibu mipango ya Israel kujiondoa katika eneo la Gaza watajaribu kuingia katika maeneo nyeti ya Jerusalem kesho Jumapili.
Polisi wa Israel wameongezwa katika eneo la Jerusalem na wamesema watawazuwia wanaharakati wa Kiyahudi kujaribu kuingia katika maeneo hayo ambayo ni matakatifu kwa Waislamu yanayojulikana kama al – Haram al- Sharif na kwa upande wa Wayahudi yanajulikana kama Temple mount.
Waziri wa usalama wa ndani wa Israel Gideon Ezra ameiambia radio ya Israel kuwa anahofu kuwa wanaharakati wa Kiyahudi watataka kuchochea hali ya wasi wasi katika maeneo hayo, ili kuharibu mpango wa kujiondoa, mpango ambao unalenga kuwaondoa walowezi wa Kiyahudi kutoka Gaza kuazia mwezi Julai.
Zaidi ya Wapalestina 10,000 wameandamana , baadhi walibeba biramu linaloonyesha mchoro wa eneo hilo takatifu, walifanya maandamano katika maeneo matatu tofauti katika mji wa ukingo wa magharibi wa Ramallah na ukanda wa Gaza.