1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gavana wa Meru anusurika kuondolewa madarakani

9 Novemba 2023

Kaunti ya Meru nchini Kenya inafungua ukurasa mpya baada ya gavana wake Kawira Mwangaza kusalimika kwa Mara ya pili jaribio la kumvua madaraka katika kipindi cha mwaka mmoja.

https://p.dw.com/p/4YbuW
Kenia Frauen Politik 2007
Picha: Roberto Schmidt/AFP/Getty Images

Gavana Mwangaza aliandamwa na madai na mashtaka saba ya uongozi mbaya na matumizi mabaya ya madaraka ambayo yametupiliwa mbali na Baraza la Seneti.

Spika wa Seneti ya Kenya Amason Kingi anatazamiwa kuwasiliana rasmi na mwenzake wa Bunge la kaunti ya Meru Ayub Bundi kumfahamisha uamuzi wa baraza hilo la Taifa.

Kwa upande wake gavana Mwangaza amewaomba radhi viongozi na wakaazi wa Meru na kuahidi kuwa na mwanzo mpya.

Tangu mwaka 2013, wawakilishi wa wadi kote nchini wamejaribu kusukuma mchakato wa kuwavua madaraka magavana 11 na manaibu wao lakini hadi kufikia sasa ni wawili pekee ambao ni Ferdinand Waititu na Mike Mbuvi Sonko ndiyo wametimuliwa.