Gates ataka kuimarishwa vita dhidi ya Malaria
19 Aprili 2018Matangazo
Vifo vitokanavyo na Malaria vimekuwa vikipungua tangu mwaka 2000, lakini vianza kuongezeka tena mwaka 2016 kutokana na kudorora kwa juhudi za kupambana na maradhi hayo yanayoenezwa na mbu. Bill Gates alikuwa akizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu Malaria unaofanyika mjini London, Uingereza.
Takwimu zinaonyesha kuwa Malaria iliwauwa watu 445,000 mwaka 2016, wengi wao wakiwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5, na wanawake wajawazito. Hali kadhalika, mwaka huo ulishuhudia visa vipya vya maambukizi milioni 216, asilimia 90 ya visa hivyo vikiripotiwa barani Afrika.
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri: Mohammed Abdulrahman