Gamescom kuimarisha utamaduni wa michezo ya kidijitali
Idadi kubwa ya watengenezaji michezo ya kompyuta na vidio wanavutiwa na tamasha la Gamescon, linalofanyika kila mwaka katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Cologne. Angalia picha za tamasha la mwaka huu.
Mavazi ya kuvutia
Tamasha la mwaka huu la Gamescom limefunguliwa rasmi Jumanne, Agosti 22, na litaendelea hadi Jumamosi, Agosti 26. Tamasha la Gamescom linaingia mwaka wake wa tisa, na linatarajiwa kuvutia wageni wengi zaidi mwaka huu kuliko idadi ya mwaka uliopita ya wageni 345,000. Baadhi ya watu wanaohudhuria tamasha hili huvaa nguo zinazofanana na watu au viumbe vya kwenye michezo hiyo.
Idadi inaongezeka
Kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu la Gamescom la mjini Cologne ni "tucheze pamoja." Zaidi ya waonyeshaji 900 kutoka nchi 50 tofauti wameleta maonyesho yao ya michezo ya computer katika tamasha la mwaka huu la Gamescom. Tamsha hilo hufanyika katika ukumbi wenye urefu wa mita za mraba 200,000. Pichani anaonekana mtu alievalia vazi la Batman.
Wazimu wa VR
Gamescom ni moja ya hafla kubwa kwa mwaka mzima, kwa watengenezaji wa michezo ya kompyuta. Wengi wao wanakuja kwenye tamasha hilo kuonyesha michezo yao mipya walioitengeza. Katika picha hii, waliohudhuriaji wanafurahia michezo ya vidio inayojulikana kama 'Virtual Reality' inayoangaliwa kwa miwani maalumu.
Umaarufu unaozidi kuongezeka
Michezo ya kompyuta na vidio imeongezeka umaarufu katika miongo ya hivi karibuni. Zaidi ya watu bilioni moja kwa sasa wanatajwa kucheza michezo hiyo kila siku. Hilo limewaongezea fursa za kujipatia kipato zaidi watengenezaji michezo hiyo. Mapato ya sekta hiyo yanatabiriwa kuongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka 2018.
Biashara inayosafirishwa ulimwenguni kote
Sambamba na tamasha hilo, kuna makongamano kadhaa yanayofanyika mjini Cologne, pamoja na hafla nyenginezo zinazotoa fursa kwa wapenzi wa michezo ya kompyuta na vidio. Wengi wa waonyeshaji wa michezo mipya wanatoka nchi za nje, na hivyo kulifanya kuwa tamasha la kimataifa. Pichani anaonekana mtu akiwa amepanda sanamu la dragoni siku ya ufunguzi wa tamasha la Gamescom.
Kibonzo anaepedwa zaidi
Pichani anaonekana mhudhuriaji akipiga picha na kibonzo wa mchezo maarufu wa Super Mario. Super Mario Bros. ni moja wapo ya michezo maarufu sana ya vidio kuwahi kutengenezwa.
Ujerumani bado iko nyuma
Ingawa Ujerumani inashika nafasi ya tano katika soko la dunia la michezo ya kompyuta na vidio, bado iko nyuma ikilinganishwa na nchi nyingine hasa katika kutengeneza mazingira mazuri kwa watengenezaji wa michezo hiyo. Mauzo ya michezo iliyotengenezwa Ujerumani ni asilimia 6 ya mauzo jumla ya ndani ya nchi. Nchi kama Canada, Ufaransa, Uingereza, Italia au Poland ziko mbele zaidi.