Mgawanyiko unazidi kushuhudiwa miongoni mwa wanasiasa wa Kenya baada ya wabunge kutoka Kenya Kwanza kumtuhumu Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua kwa kufanya mambo yanayouathiri umoja wa kitaifa, hali iliyomuibua Gachagua mwenyewe akimtaka Rais William Ruto kuingilia kati ili afanye kazi yake ya kuudumia umma. Sudi Mnette alizungumza na Mchambuzi wa siasa za Kenya Bobby Mkangi juu ya hili.