G7 kutangaza marufuku kwa almasi ya Urusi
6 Desemba 2023Mkutano huo wa kilele wa viongozi wa G7 unaofanyika kwa njia ya video pia utajadili kuhusu ukomo wa bei ya mafuta.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine anatarajiwa kuhudhuria sehemu ya kwanza ya mkutano huo utakaoongozwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida.
Soma zaidi: Marekani, washirika wazidisha shinikizo la kiuchumi kwa Urusi
Ikiwa karibu miaka miwili baada ya uvamizi wa Urusi, dalili zinaongezeka kuwa uungaji mkono wa Ukraine kutoka kwa Magharibi unapungua wakati ambapo mapambano ya jeshi la Urusi yakionekana kuyumba, na wakati mapato ya mafuta ya Rais Vladmir Putin yakiimarika.
Zelensky jana alifanya uamuzi wa ghafla wa kutohudhuria mkutano mwengine wa vidio hapo jana na maseneta wa Marekani.
Bunge la Marekani limegawanyika zaidi kuhusu uungaji mkono wa Ukraine kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote katika vita hivyo, huku nchi hiyo ikionekana kuumaliza haraka msaada wa kujeshi uliotolewa na Marekani mpaka sasa.