UchumiBrazil
G20 yaweka mikakati kuwatoza kodi matajiri wakubwa duniani
27 Julai 2024Matangazo
Katika taarifa yao, mawaziri hao wamesema wanasaka uwiano wa kimataifa na ushirikiano zaidi juu ya kuziba mianya ya matajiri wakubwa kukwepa kulipa kodi.
Brazil inayoshikilia urais wa kupokezana wa kundi la G20, ilitoa pendekezo la kuwatoza ushuru wa asilimia mbili watu wenye utajiri unaozidi dola bilioni moja za Kimarekani.
Soma pia: Oxfam: Matajiri duniani waongeza utajiri wao
Licha ya kutokubaliana kuhusu kiwango maalum cha ushuru, waziri wa fedha wa Brazil Fernando Haddad amesema wamepiga hatua muhimu.
Pendekezo la kuwatoza ushuru watu wenye utajiri uliopindukia limeibua mgawanyiko miongoni mwa nchi wanachama wa G20.
Ufaransa, Uhispania na Afrika Kusini zimeunga mkono japo Marekani imepinga pendekezo hilo.