Freidrich Merz aunga mkono mazungumzo ya kibiashara na Trump
2 Januari 2025Merz ameyasema hayo wakati akijibu matamshi makali yaliyotolewa na Trump kuhusu masharti magumu ya biashara.
Akizungumza na shirika la habari la Ujerumani la dpa, Merz anayeongoza kwenye kura ya maoni ya kuchukuwa nafasi ya ukansela, amesema Ujerumani inahitaji ajenda chanya na Marekani itakayoifaidisha Marekani na watu wa Ulaya.
Soma pia: Steinmeier alivunja bunge na kupisha njia ya uchaguzi wa mapema
Ameeleza kuwa makubaliano mapya ya kibiashara yanaweza kuikinga Ulaya na hatari ya ongezeko kubwa la ushuru.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, anayetarajiwa kuapishwa rasmi madarakani Januari 20 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya Ujerumani kufanya uchaguzi wa mapema Februari 23, alisitisha mazungumzo ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani yaliyopendekezwa wakati wa muhula wake kwa kwanza wa urais na badala yake kuwa na mivutano kadhaa ya kibiashara na Umoja huo.