1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Franz Beckenbauer matatani

14 Septemba 2016

Franz Beckenbauer, ambae alisema alifanyakazi bila malipo kama mwenyekiti wa kamati ya matayarisho ya fainali za kombe la dunia, alipokea zaidi ya euro milioni tano,lilisema gazeti la Spiegel la Jumatano(14.09.2016).

https://p.dw.com/p/1K1xo
Franz Beckenbauer
Franz BeckenbauerPicha: picture-alliance/dpa/M. Müller

Mchezaji huyo maarufu wa kandanda nchini Ujerumani pia alitaka kuficha kiwango hicho cha fedha kwa maafisa wa kodi , jarida hilo lilisema, ikiwa ni tukio la hivi karibuni kabisa la kuleta fadhaa kwa Beckenbauer, ambaye anachunguzwa na maafisa wa Uswisi kuhusiana na madai ya rushwa katika kuhusiana na kupata Ujerumani kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2006.

Welttag des Kusses Franz Beckenbauer und Sepp Maier
Franz Beckenbauer (kati)kama nahodha wa Ujerumani magharibi 1974Picha: picture alliance/dpa/W. Baum

Ugunduzi wa hivi karibuni umezusha hasira kutoka kwa kiongozi wa shirikisho la kandanda la Ujerumani Reinhard Grindel , ambaye amemshutumu Beckenbauer anayejulikama nchini Ujerumani kwa jina la utani kama "kaiser" mwenye umri wa miaka 71, kwa kudanganya na kupotosha umma.

Kwa mujibu wa jarida la Spiegel, idadi hiyo ya fedha ilipatikana kutoka mchango wa euro milioni 12 zilizotolewa na mfadhili wa kombe la dunia, kampuni ya kubashiri ya Oddset.

"Tunafahamu kwamba Franz Beckenbauer alifanyakazi pamoja na Oddset katika mfumo wa kombe la dunia. lakini hatukufahamu kwamba alipata kiasi cha euro milioni 5.5 kutoka katika bajeti ya matayarisho ya kombe la dunia mwaka 2006," Grindel alisema katika taarifa.

Wolfgang Niersbach und Franz Beckenbauer
Beckenbauer(kulia) na rais wa zamani wa shirikisho la kandanda la Ujerumani Wolfgang niersbachPicha: picture-alliance/AP Photo/F. Augstein

"Bila shaka , kutokana na hali hii , hatuwezi kusema kwamba alifanyakazi bila malipo katika kamati hiyo ya maandalizi," kiongozi huyo wa DFB alisema katika taarifa kutoka Athens , ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa UEFA.

Beckenbauer hakuwasilisha idadi hiyo ya fedha kwa maafisa wa kodi kwa miaka minne, kwa mujibu wa jarida la Spiegel.

Lakini kufuatia uchunguzi wa maafisa wa kodi , DFB iliamuriwa kulipa uero milioni moja kwa kuzuwia kodi kwa kiwango hicho cha mwaka 2010.

Beckenbauer hatimaye alilipa kodi hiyo iliyotakiwa kulipwa na DFB.

Beckenbauer alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 1974 katika kombe la dunia na aliifunza timu hiyo ambayo hatimaye ilishinda kombe hilo mwaka 1990 nchini Italia.

Italien, Deutsche Fußballnationalmannschaft wird Weltmeister 1990
Franz Beckenbauer akiwa kocha wa mabingwa wa dunia Ujerumani 1990Picha: picture-alliance/dpa/F. Kleefeldt

Lakini hadhi yake imeharibiwa na jukumu lake katika kashfa inayoendelea kuhusiana na kupewa Ujerumani hadi ya kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.

Maafisa wa Uswisi wanafanya uchunguzi dhidi yake, pamoja na watu wengine watatu waliokuwa wanachama katika kamati hiyo ya matayarisho, kuhusiana na madai ya udanganyifu, uhalifu wa kiutendaji, kutakatisha fedha na ubadhirifu."

Uchunguzi huo umekuja baada ya ripoti ya jarida hilo la Spiegel Oktoba mwaka jana kwamba fedha zilizohifadhiwa kwa siri zaidi ya faranga za Uswisi milioni 10 sawa na euro milioni 6.7 zilitumika kununua haki ya kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2006.

Deutschland DFB neuer Präsident Reinhard Grindel
Rais wa shirikisho la soka la Ujerumani DFB Reinhard GrindelPicha: Getty Images/Bongarts/A. Grimm

Fedha hizo zinadaiwa zilitoka kwa Robert Louis-Dreyfus , bosi za zaani wa kampuni ya Adidas , kwa ombi la Beckenbauer, na zikikabidhiwa mwaka 2000, muda mfupi kabla ya Ujerumani kupewa uenyeji wa fainali za mwaka 2006 kwa wingi mdogo wa kura.

Mwezi Mei tume huru ya uchunguzi iliyoundwa na shirikisho la kandanda nchini Ujerumani DFB ilisema haiwezi kuondoa uwezekano kwamba Ujerumani ilinunua kura kuweza kupata kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 2006. Becekenbauer amekuwa wakati wote akikana tuhuma hizo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Yusuf , Saumu