Finland yatumai kukubaliana na Uturuki kuhusu NATO
17 Mei 2022Matangazo
Rais wa Uturuki Recep Tayip Erdogan ametishia kuzuia utanuzi wa jumuiya hiyo akizituhumu Finnland na Sweden kwa kuwaficha wanamgambo wa kituruki wa chama cha Kurdistan Workers, ambao wameendeleza uasi wa miongo kadhaa dhidi ya dola la Uturuki.
Sweden imesitisha uuzaji wa silaha kwa Uturuki tangu 2019 kuhusiana na harakati ya kijeshi ya Uturuki katika nchi jirani ya Syria.
Wakati hayo yakiarifiwa, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema ana imani Finnland na Sweden zitajiunga haraka na NATO licha ya upinzani kutoka kwa Uturuki.
Baerbock aidha amesema ikiwa mchakato utachelewa wanachama wa NATO watazipa nchi hizo hakikisho maalumu la usalama.
Chanzo: reuters