1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Finland kuwasilisha rasmi ombi la kujiunga na NATO

15 Mei 2022

Serikali ya Finland Jumapili ilitangaza kuwa itawasilisha ombi la kujiunga na muungano wa kujihami wa NATO baada ya chama tawala nchini humo kuunga mkono hatua hiyo.

https://p.dw.com/p/4BKa6
Helsinki | Pressekonferenz zum Beitritt Nato Mitgliedschaft Finnland | Sauli Niinistö
Picha: Heikki Saukkomaa/Lehtikuva/dpa/picture alliance

Bunge la Finland linatarajiwa kuunga mkono uamuzi huo katika siku chache zijazo.

Uamuzi huu unakuja wakati ambapo Urusi inaivamia Ukraine na inaonyesha mabadiliko makubwa katika msimamo wake wa muda mrefu wa kutoegemea upande wowote.

Wasoshalisti Sweden kuunga mkono uamuzi wa kujiunga na NATO

Rais wa Finland Sauli Niinisto alisema anakubaliana na serikali na kwamba atashauriana na bunge kabla kutangaza uamuzi huo.

"Hii ni siku ya kihistoria. Enzi mpya inafunguka," alisema Niinisto katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari alipokuwa na Waziri Mkuu Sanna Marin.

Helsinki | Pressekonferenz zum Beitritt Nato Mitgliedschaft Finnland | Sanna Marin
Waziri Mkuu wa Finland Sanna MarinPicha: Heikki Saukkomaa/Lehtikuva/dpa/picture alliance

Chama cha Kisoshalisti cha Sweden kinatarajiwa pia kuunga mkono uamuzi huo wa kujiunga na NATO siku ya Jumapili.

Wasoshalisti wa Sweden kwa muda mrefu wamekuwa wakipinga uamuzi huo wa kujiunga na NATO ila hatua ya Urusi kuivamia Ukraine ni jambo lililozua mjadala nchini Sweden kuhusiana na kujiunga na muungano huo.

Waziri Mkuu wa Finland Marin alisema kujiunga na NATO pamoja na Sweden ni hatua muhimu sana. "Ni muhimu sana kwamba tuna mwelekeo mmoja na tunakwenda kwa kasi sawa," alisema Marin.

Katibu Mkuu wa NATO Mircea Geoana alisema Jumapili Finland na Sweden tayari ni washirika wa karibu wa muungano huo wa kujihami.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock naye alisema Ujerumani inataka uidhinishwaji wa nchi hizo uharakishwe. Kuidhinishwa kwa nchi hizo ni jambo linaloweza kuchukua hata mwaka mmoja mzima.

"Nchi hizi mbili zikiamua kujiunga zinaweza kujiunga kwa haraka sana," alisema Baerbock.

Urusi kulipiza kisasi kutokana na upanuzi wa NATO

Wakati huo huo Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO imepinga hatua ya nchi hizo mbili za Nordic kujiunga na muungano huo. Geoana lakini amesema ana imani kuwa wanaweza kuafikiana na Uturuki kuhusiana na suala hilo.

Russland | Militärparade am 9. Mai in Moskau | Wladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Kirill Kudryavtsev/AFP

Urusi imeahidi kulipiza kisasi kuhusiana na NATO kuupanua muungano huo ingawa haijatangaza jinsi itakavyolipiza.

Hapo Jumamosi, Rais wa Finland alisema alimwambia Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusiana na mpango wa nchi yake kujiungana na muungano huo wa nchi za Magharibi.

Kuliingana na taarifa ya Kremlin, Putin alimwambia Niinisto kuwa Urusi si kitisho kwa Finland ila uanachama wake kwa NATO unaweza kuathiri mahusiano ya nchi hizo mbili.

Chanzo: https://bit.ly/3FPY4E0