SiasaFinland
Finland kujiunga rasmi na NATO siku ya Jumanne
3 Aprili 2023Matangazo
Tangazo hilo limezusha tahadhari kutoka Urusi ambayo imesema itaimarisha hatua zake za kiulinzi karibu na mpaka wao wa pamoja na nchi hiyo, ikiwa Nato itapeleka kikosi chochote cha wanajeshi katika ardhi ya mwanachama wake huyo mpya.
Stoltenberg amesema Uturuki ambayo ni mwanachama wa mwisho kuidhinisha Finnland itakabidhi idhini rasmi kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kesho. Rais wa Finland Sauli Niinisto na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Antti Kaikkonen watashiriki sherehe hiyo pamoja na waziri wa mambo ya nje Pekka Haavisto.
Katibu mkuu wa NATO pia amezungumzia matumaini ya kuiona Sweden nayo pia ikijiunga na jumuiya hiyo hivi karibuni.