Mgombea wa AfD atabiriwa ushindi Bitterfeld-Wolfen
8 Oktoba 2023Mgombea wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Ujerumani (AfD), Henning Dornack, anatarajiwa kuibuka na ushindi katika duru ya pili ya umeya kwenye mji wa Bitterfeld-Wolfen, ulio katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani, Saxony-Anhalt. Mji huo ni mdogo, wenye wakazi wapatao 37,000, lakini viongozi wa AfD wana matumaini kwamba ushindi wao dhidi ya meya wa sasa, Armin Schenk wa chama cha CDU, unaweza kuendeleza mfululizo wa mafanikio ya ushindi katika chaguzi zijazo ambazo zinaweza kukisogeza chama chao katika kitovu cha siasa za Ujerumani.Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kumfanya Dornack kuwa mwanachama wa kwanza wa AfD kuchaguliwa kuwa meya wa katika mji mkubwa nchini Ujerumani.Katika duru ya kwanza ya uchaguzi majuma mawili yaliyopita, Dornack alipata asilimia 34 ya kura huku Schenk akipata asilimia 29.