1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EURO 2024: Germany yatinga robo fainali

30 Juni 2024

Timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani imefuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2024, baada ya miaka minane, lakini bado hali ni tete.

https://p.dw.com/p/4hgnN
Euro2024: Mchezaji wa Ujerumani Jamal Musiala akishinda bao la pili dhidi ya Denmark
Euro2024: Mchezaji wa Ujerumani Jamal Musiala akishinda bao la pili dhidi ya DenmarkPicha: Dean Mouhtaropoulos/Getty Images

Wenyeji walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Denmark licha ya mechi kusitishwa kwa muda kutokana na  dhoruba na radi.

Kocha wa  Ujerumani Julian Nagelsmann licha ya ushindi aliitaja mechi hiyo kuwa "ya ajabu" baada ya matokeo mara mbili kuamuliwa na mfumo wa teknolojia ya VAR kuwapendelea Ujerumani.

Ujerumani na Uswisi wamefuzu katika hatua ya robo fainali huku mabingwa watetezi Italia na Denmark wakifungasha virago na kuyaaga mashindano hayo. Hii leo England itashuka dimbani dhidi ya Slovakia kisha Uhispania ikipige na Georgia.