EU yaweka mpango wa kupunguza matumizi ya gesi
20 Julai 2022Matangazo
Katika rasimu ya mpango huo, ambao unaweza kubadilika wakati wowote, Halmashauri Kuu hiyo ya Umoja wa Ulaya imezihimiza nchi wanachama kuendelea na hatua za hiari za kupunguza matumizi ya gesi ili kuepuka mgororo.
Hata hivyo, baadhi ya nchi za Umoja huo zimeonyesha wasiwasi wa kutokea dharura kutokana na usambazaji mdogo wa gesi.
Shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia limetoa tahadhari kwamba juhudi za Umoja wa Ulaya za kutafuta gesi mbadala huenda zisifanikiwe kuelekea msimu wa baridi, na kutoa wito kwa nchi hizo kupunguza matumizi yake ya gesi.
Umoja wa Ulaya umejitahidi kuondokana na utegemezi wake wa nishati ya Urusi, huku mwaka jana umoja huo ukiagiza asilimia 40 ya gesi yake kutoka Moscow.