SiasaJamhuri ya Moldova
EU yampongeza Maia Sandu kwa ushindi wa urais, Moldova
4 Novemba 2024Matangazo
Katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, von der Leyen, amemwambia rais huyo kwamba kunahitajika ukakamavu wa kipekee kukabiliana na changamoto alizokumbana nazo katika uchaguzi huo.
Moldova yapiga kura katika uchaguzi tete kuhusu mustakabali wa EU
von der Leyen pia ameelezea furaha ya kuendelea kushirikiana na rais Sandu kuelekea mustakabali wa Ulaya kwa Moldova na watu wake.
Moldova iliingia katika duru ya pili ya uchaguzi
Ushindi wa Sandu unakuja baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais jana Jumapili.
RaisSandu, alipata asilimia 42.5 katika duru ya kwanza, huku Alexandr Stoianoglo, anayeungwa mkono na Urusi, akipata asilimia 26.