EU yaishutumu Belarus kwa ukandamizaji
26 Januari 2024Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel, amesema Umoja huo unashtumu vikali wimbi la ukandamizaji la hivi karibuni dhidi ya wafungwa wa zamani wa kisiasa waliosalia Belarus pamoja na jamaa za wafungwa hao.
Marekani yaahidi hatua zaidi dhidi ya Belarus
Marekani pia imeshtumu mashambulizi hayo makubwa yanayofanywa na utawala wa Belarus dhidi ya haki za binadamu na majaribio ya kuzima matarajio ya kidemokrasia ya watu wa Belarus.
Soma pia:Putin na Lukashenko wafanya mazungumzo Urusi
Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller, amesema wataendelea kuuwajibisha utawala wa Belarus kupitia vikwazo na njia nyinginezo, kwa ukandamizaji wake mkali wa ndani pamoja na uungaji wake mkono wa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.