Ulaya yakubali kuisaidia Athens kuwafukuza wahamiaji zaidi
14 Machi 2023Serikali ya Ugiriki na mamlaka inayosimamia mipaka ya Umoja wa Ulaya, Frontex imetia saini makubaliano ya ushirikiano wa pamoja mjini Athens hii leo ambapo mamlaka hiyo itaisaidia Ugiriki kuwarejesha nyumbani wahamiaji wasiostahili kuomba hifadhi nchini humo.
Hatua hiyo ya kuwarejesha watu nyumbani kwa hiari inaungwa mkono chini ya makubaliano hayo kati ya Wizara ya uhamiaji ya Ugiriki na mamlaka ya Frontex.
Wizara hiyo imesema, Umoja wa Ulaya unaojumuisha nchi wanachama 27 ikiwemo Ugiriki inapaswa kwa pamoja kujadili suala hilo na kuongeza idadi ya wahamiaji wanaorejeshwa katika mataifa yao husika.
Waziri wa Uhamiaji Notis Mitarachi, amesema idadi ndogo ya watu ambao hawapaswikuomba hifadhi wanaorejeshwa nyumbani inaondoa uadilifu katika mfumomzima wa kuomba hifadhi.