Ethiopia yatoa onyo juu ya uchunguzi wa vita vya Kaskazini
15 Februari 2023Katika ripoti yake ya kwanza iliyochapishwa Septemba mwaka jana, Tume ya Watalaamu wa Haki za Binaadamu kuhusu Ethiopia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilisema ilikuta ushahidi wa ukiukaji kutoka pande zote ambao unaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Waasi wa Tigray waanza kuzisalimisha silaha zao nzito
Serikali ya Ethiopia iliipinga ripoti hiyo na imeanzisha juhudi za kidiplomasia ili kupata uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa katika jaribio lake la kuizuia tume hiyo kuendelea na kazi yake.
Jeshi la kikanda lajiondoa mji wa kimkati wa Shire-Tigray
Naibu waziri mkuu wa Ethiopia na Waziri wa Mambo ya Kigeni Demeke Mekonnen amesema tume hiyo huenda ikahujumu mchakato wa amani ulioongozwa na Umoja wa Afrika na utekelezwaji wa Makubaliano ya Amani ya Pretoria kwa kutumia maneno ya uchochezi.