1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroEthiopia

Ethiopia yarundika wanajeshi kwenye eneo la Amhara

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Jimbo hilo linakumbwa na uasi wa wapiganaji wenye silaha kwa zaidi ya mwaka mmoja wakati serikali ilipotangaza hali ya hatari.

https://p.dw.com/p/4lRrJ
Mnamo Agosti mwaka jana, serikali ilitangaza hali ya hatari huko Amhara
Mnamo Agosti mwaka jana, serikali ilitangaza hali ya hatari huko Amhara Picha: Ethiopian Prime Minister's Office/AA/picture alliance

Chanzo cha usalama kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, Jumamosi (05.10/2024), kwamba watumishi kadhaa wa umma wanaoshukiwa kushirikiana na wapiganaji hao wa FANO wamekamatwa pia. Hata hivyo, taarifa hiyo haikusibitishwa na duru isioegemea upande wowote, kwani mamlaka huzuia ufikiaji wa eneo hilo.

Wafano, wanamgambo wa jadi kutoka kabila la Amhara, ambaloo ni la pili kwa idadi ya watu nchini Ethiopia, walichukua silaha dhidi ya serikali kuu mnamo Aprili 2023 katika eneo hilo lenye wakaazi milioni 23. Mnamo Agosti mwaka jana, serikali ilitangaza hali ya hatari huko Amhara.

Wiki hii, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Internatinal lilituhumu kile lilichoelezea kuwa ni kamatakamata ya kiholela ya watu, wakiwemo wasomi, kwenye mkoa wa Ahmara.