Abiy aonya kudhalilisha taifa lolote linalolenga kuwavuruga
9 Septemba 2024Ethiopia ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika imetumbukia kwenye mzozo na nchi jirani ya Somalia kufuatia makubaliano ya bandari iliyotia saini na eneo lililojitenga la Somaliland.
Uhusiano kati ya Ethiopia na Misri pia unayumba kutokana na hatua ya Ethiopia ya kujenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme katika Mto Nile. Misri ilipeleka vifaa vya kijeshi nchini Somalia mara baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Cairo na Mogadishu.
Misri pia imejitolea kupeleka wanajeshi nchini Somalia mwaka ujao chini ya mpango mpya unaoongozwa na Umoja wa Afrika, ambao utachukua nafasi ya kikosi cha sasa cha kulinda amani (ATMIS).
Ethiopia kwa sasa ni mchangiaji mkuu wa kikosi cha sasa cha kulinda amani kinachovisaidia vikosi vya Somalia katika mapambano yake dhidi ya kundi la kigaidi la Al-Shabab.