Ethiopia yahofia ujumbe mpya wa amani wa Somalia
29 Agosti 2024Matangazo
Hii ni baada ya Misri kusema kuwa ilituma msaada wa kijeshi kwa taifa hilo linalokumbwa na migogoro.
Ujumbe huo mpya, unaojulikana kama AUSSOM, unatazamiwa mwezi Januari kuchukua nafasi ya kikosi cha kulinda amani cha AU ambacho kilitumwa nchini Somalia kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab.
Wasiwasi huo unashuhudiwa baada ya Misri, ambayo kwa muda mrefu imekuwa katika msuguano na Ethiopia, kutuma vifaa vya kijeshi nchini Somalia katika hatua ambayo huenda ikazidisha mvutano kati ya Cairo na Addis Ababa.
Misri na Ethiopia zimekuwa na mzozo kwa miaka mingi kuhusu mradi wa bwawa kubwa la Ethiopia kwenye mto Nile, ambao Misri inasema unatishia usalama wake wa upatikanaji wa maji.