Ethiopia na Eritrea zatia saini mkataba wa urafiki
17 Septemba 2018Matangazo
Miezi miwili baada ya kutiliana saini makubaliano ya kihistoria ya kurejesha amani kati yao, Ethiopia na Eritrea zimetiliana saini mkataba wa urafiki.
Rais Isaias Afwerk wa Eritrea na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, walitia saini mkataba huo mjini Jeddah mbele ya mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Al Saud.
Hata hivyo, hakuna maelezo ya undani juu ya mkataba huo yaliyotolewa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia alihudhuria sherehe hiyo ya kutia saini.