Ethiopia imeshindwa kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu
6 Agosti 2024Shirika hilo limeeleza hayo wakati likilaani kukamatwa kwa kaka wa kiongozi wa chama cha upinzani cha OLF aliyeuwawa Bate Urgessa mwezi Aprili.
Amnesty International limesema licha ya mahakama kuamuru mtu huyo aachiliwe huru mwezi Juni, bado anashikiliwa.
Shirika hilo limeongeza kuwa licha ya kukoma kwa vita vilivyodumu kwa miaka miwili katika mkoa wa Tigray Novemba 2022, bado kuna mizozo mingi ikiwemo katika majimbo ya Amhara na Oromia.
Soma pia:Visa vya utekaji nyara vyaripotiwa Oromia na Amhara nchini ethiopia
Limebainisha kuwa, madai ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuwa jeshi lake halifanyi mauaji ya kimbari yanaonesha jinsi serikali inavyoendelea kukanusha uhalifu wake wa sasa na wa zamani.
Limeyataka mataifa washirika barani Afrika na vyombo vingine vya haki kuchukua hatua ili kuchunguza tuhuma za uhalifu ukatika eneo la Amhara.