1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachama wa AfD wachagua viongozi wao leo

29 Juni 2024

Wanachama cha mrengo wa kulia AfD wamekusanyika huko katika mji wa magharibi wa Essen wa Ujerumani kwa siku mbili kongamano la chama, huku umati mkubwa wa waandamanaji ukikabiliana na idadi kubwa ya polisi nje ya ukumbi.

https://p.dw.com/p/4hfLU
Ujerumani | Mkutano wa chama cha AfD huko Essen | Chrupalla na Weidel
Wenyeviti wenza wa AfD Alice Weidel na Tino Chrupalla walipozungumza mwanzono mwa mkutano wao huko huko Grugahalle Essen.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Mapema mwezi huu AfD iliibuka kwa kushika nafasi ya pili katika uchaguzi wa bunge la Ulaya, na ipo katika maandalizi ya chaguzi za majimbo matatu ya mashariki mwa Ujerumani, huku kura za maoni zikionesha chama hicho chenye kupinga uhamiaji kuwa na nafasi kubwa.

Mwenyekiti mwenza wa AfD, Tino Chrupalla amesikika akijigamba mbele ya wajumbe washiriki kuwa wao wanaongoza katika eneo la mashariki na wanataka kushinda katika uchaguzi ujao ili kutanua wigo na kuendeleza nafasi yao.

AfD iliondolewa utambuzi na Kundi la wapigia chapuo demokrasia katika bunge la Ulaya kufuatia matamshi aliyekuwa mgombea wake wa katika uchaguzi wa bunge la Ulaya, Maximilian Krah, kwamba siyo wanachama wote wa kundi la kijeshi la SS lililohudumu chini ya Adolf Hitler na chama cha Wanazi kwa wakati huo walikuwa wahalifu.