1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Erdogan kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7, Italia

30 Mei 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atahudhuria mkutano wa kilele wa kundi la G7 utakaoandaliwa mwezi ujao katika hoteli ya kifahari ya Borgo Egnazia ilioko eneo la Kusini mwa Italia, Puglia, kuanzia Juni 13-15

https://p.dw.com/p/4gR50
Mawaziri wa mambo ya nje na maendeleo wa kundi la G7 katika picha ya pamoja Liverpool nchini Uingereza mnamo Desemba 12,2021
Mawaziri wa mambo ya nje na maendeleo wa kundi la G7Picha: Olivier Douliery/AP Photo/picture alliance

Mwezi Aprili, shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa nchi kadhaa za Afrika na Amerika Kusini zimealikwa katika kile kinachoitwa mikutano ya uhamasishaji, na wiki hii Italia imesema kuwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, pia atahudhuria.

Mwanafalme wa Saudi Arabia pia anatarajiwa kuhudhuria mkutuno huo wa G7

Vyanzo vilivyo karibu na maandalizi ya mkutano huo vimeiarifu Reuters kuwa mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman pia anatarajiwa kuhudhuria ijapokuwa hakujakuwa na thibitisho rasmi.

Papa Francis kuzungumzia changamoto za akili ya kubuni

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis pia atakuwa miongoni mwa watakaohudhuria mkutano huo ambapo atajadili changamoto zinazosababishwa na matumizi ya akili ya kubuni.