MigogoroUturuki
Erdogan: Wanachama 1,000 wa Hamas wanapokea matibabu Uturuki
14 Mei 2024Matangazo
Rais Erdogan ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.
Kiongozi huyo wa Uturuki hata hivyo hakutoa maelezo zaidi juu ya sehemu walikojeruhiwa wanachama hao wa Hamas au jinsi walivyofika Uturuki.
Soma pia: Hamas yakubali kusitisha mapigano, Israel yaishambulia Rafah
Erdogan amewahi kuieleza Hamas kama kundi la ukombozi linalotetea haki za Wapalestina.
Hata hivo, Marekani, Uingereza, Israel na mataifa mengine yenye nguvu yameliorodesha Hamas kama kundi la kigaidi.