Erdogan huenda akamualika Assad kwa mazungumzo Uturuki
7 Julai 2024Matamshi ya Erdogan yanakuja baada ya mvutano ulioshuhudiwa wiki iliyopita, wakati magenge ya watu yalipomiminika mitaani yakiharibu biashara na mali za raia wa Syria mjini Ankara.
Uturuki ilikuwa na nia ya kuuangusha utawala wa Rais Bashar al Assad wakati vita vya Syria vilipoanza mwaka 2011 kwa kuwaunga mkono waasi waliotaka Bashar aondoke uongozini.
Erdogan hajaondoka uwezakano wa kurudisha uhusiano na Syria
Lakini hivi maajuzi Erdogan alisema huenda akayasawazisha mahusiano yake na Assad wakati serikali yake ikijaribu kuhakikisha Wasyria wanaotaka kurudi nyumbani kwa hiari wanarejea salama.
Akizungumza na waandishi habari Erdogan amesema viongozi kama rais wa Urusi Vladimir Putin wameahidi kuwa mpatanishi katika mkutano wa viongozi hao wawili nchini Uturuki.