1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan amshukuru Putin kwa kurefusha mkataba wa nafaka

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Rais wa Uturuki, RecepTayyip Erdogan amefanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladmir Putin na kujadili namna ya kuboresha mahusiano kati ya mataifa yao

https://p.dw.com/p/4PF1U
Putin empfängt Erdogan in Sotschi
Picha: Vladimir Smirnov/Sputnik/REUTERS

Katika mazungumzo yao ya leo Jumamosi, yaliyofanyika kwa njia ya simu, viongozi hao wamejadili pia juu ya yanayoendelea katika vita nchini Ukraine.

Soma zaidi: Erdogan kukutana tena na Putin kuhusu Ukraine

Rais Erdogan katika mazungumzo hayo ameelezea umuhimu wa kuumaliza mzozo kati ya Urusi na Ukraine kwa njia ya mazungumzo haraka iwezekanavyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Uturuki, Erdogan amemshukuru pia Rais Putin kwa mtazamo wake chanya katika kuurefusha mkataba wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi. 

Chanzo: RTRE