1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

England yapata ushindi wa tabu dhidi ya Serbia

17 Juni 2024

Jude Bellingham ameifungia timu ya taifa ya England bao la kipekee na la ushindi katika mechi yao ya kwanza ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2024 dhidi ya Serbia mjini Gelsenkirchen.

https://p.dw.com/p/4h75O
Euro 2024 | Serbia vs England | (0:1)
Bellingham akishangilia bao lake katika mchezo dhidi ya Serbia kwenye Kundi C ya UEFA Euro 2024 Uwanja wa AufSchalke mjini Gelsenkirchen, Ujerumani.Picha: Martin Rickett/PA Images/IMAGO

Bao la Bellingham liliwatuliza mashabiki wa England kunako dakika ya 13 ya mchezo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bukayo Saka.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye pia ameshinda Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya katika msimu wake wa kwanza akiwa na Real Madrid - alicheza vizuri na kudhihirisha ni kwanini yeye ndio nyota mpya wa timu ya taifa ya England.

Soma pia: Ufaransa, England zapigiwa upatu kubeba Euro 2024

Hata hivyo, Serbia ilijiimarisha kipindi cha pili japo walishindwa kufunga bao la kusawazisha.

Vijana wa Gareth Southgate sasa wanaongoza kundi C wakiwa na alama tatu baada ya wapinzani wao wengine Denmark na Slovenia kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mapema.

England inateremka tena uwanjani siku ya Alhamisi kucheza dhidi ya Denmark katika uwanja wa Deutsche Bank Park.