Euro 2024: Ni England au Uhispania leo?
14 Julai 2024Matangazo
Mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa saa nne usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki na saa tatu usiku kwa saa za Ulaya ya kati, inatarajiwa kuhudhuriwa na Mwanamfalme wa Uingereza William, Mfalme Felipe wa Uhispania, Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez na Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer.
Uhispania inawania kushinda ubingwa huo kwa mara ya nne ikiwa na mchezaji wake nyota Lamine Yamal aliyetimiza miaka 17 jana Jumamosi. Kwa upande wake England inayodai kuwa ndiko soka lilikozaliwa, haijawahi kushinda kombe lolote kubwa tangu walipojinyakulia kombe la dunia mnamo mwaka 1966.