Durov akubali Telegram kushirikiana na vyombo vya usalama
24 Septemba 2024Matangazo
Durov, ambaye alikamatwa nchini Ufaransa mwezi uliopita kwa tuhuma za kushindwa kuchukuwa hatua dhidi ya wahalifu kwenye mtandao wake, alisema huduma ya kutafuta taarifa ya Telegram imetumika vibaya na watu wanaouza bidhaa haramu.
Kuanzia sasa, Telegram itakuwa inawapa maafisa wa usalama taarifa kama vile nambari ya simu na anwani ya mtandaoni ya wale wanaovunja kanuni za matumizi.
Soma zaidi: Mmilki wa Telegram ashtakiwa, mtandao wake si salama
Durov, mwenye umri wa miaka 39, yuko nje kwa dhamana, lakini haruhusiwi kutoka nje ya Ufaransa.
Kukamatwa kwake kulihusishwa na kukataa kwa mtandao wake kushirikiana na vyombo vya usalama juu ya masuala ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, biashara haramu ya binaadamu na udanganyifu wa mtandaoni.