1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dunia yaonyesha mshikamano na Wamarekani, wito wa mabadiliko

1 Juni 2020

Watu wengi duniani wanafuatilia kwa wasiwasi machafuko ya kiraia yanayoendelea nchini Marekani kufuatia mauaji ya karibuni kufanywa na polisi dhidi ya wanaume na wanawake wenye asili ya Afrika nchini humo.

https://p.dw.com/p/3d6Sf
USA Proteste nach dem Tod von George Floyd | Plakate I Can't Breathe
Picha: Imago Images/ZUMA Wire/S. S: Gurbuz

Waandamanaji katika mji wa Auckland nchini New Zealand wamekusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani ambako walipiga magoti, wakiwa na mabango yenye ujumbe kama vile "siwezi kupumua" na "kirusi halisi ni ubaguzi wa rangi." 

Mamia wengine walijiunga na maandamano ya amani na ukeshaji kwingineko nchini New Zealand, ambako Jumatatu ni siku ya mapumziko.

Katika mkusanyiko katikati mwa jiji la London, Uingereza Jumapili, maelfu walijitolea kuwaunga mkono wandamanaji nchini Marekani, wakipaza sauti za "Hakuna haki! Hakuna amani!" huku pia wakipeperusha mabango yenye maneno yasemayo "wangapi wengine zaidi?"

Katika maeneo mengine pia, waandamanaji walionyesha mshikamano na wenzao wa Marekani kwa kutoa ujumbe ulioelekezwa kwa serikali za maeneo.

USA Proteste nach dem Tod von George Floyd | Plakate Black Lives Matter
Ni maandamano yaliowahusisha watu wa rangi tofauti.Picha: Reuters/L. Bryant

Nchini Brazil, mamia ya watu waliandamana kupinga uhalifu uliofanywa na polisi dhidi ya watu weusi katika maeneo ya tabaka la wafanyakazi mjini Rio de Jenairo, yanayojulikana kama favela.

Polisi ilitumia gesi ya kutoa mchozi kuwatawanya, huku baadhi yao wakisema "siwezi kupumua", wakirejea maneno aliyokuwa akiyasema Floyd.

Nchini Canada, maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaligeuka makabiliano kati ya polisi mjini Montreal na baadhi ya wandamanaji.

Polisi iliyatangaza maandamano hayo kuwa haramu baada ya kusema viripuzi kurushwa dhidi ya maafisa waliojibu kwa kutumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi.

Mataifa ya kiimla yatumia fursa kuikosoa Marekani

Katika mataifa ya kiimla, machafuko hayo yamegeuka fursa ya kupuuza ukosoaji wa Marekani dhidi ya hali zao. Televisheni ya taifa ya Iran ilikuwa ikirejea kutangaza picha ya machafuko ya nchini Marekani.

USA Proteste nach dem Tod von George Floyd | Plakate I Can't Breathe
Waandamanaji mjini New York wakiwa na bango lisemalo: "Hatuwezi kupumua."Picha: picture-alliance/XinHua/M. Nagle

Na msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni nchini humo Abbas Mousavi akatumia fursa hiyo kutoa wito wak Washington kuacha vurugu dhidi ya raia.

''Na kwa maafisa wa serikali ya Marekani na Polisi: Acheni vurugu dhidi ya watu wenu na muwaache wapumue. Ahsante,'' alisema Mousavi wakati akituhubiwa mkutano wa waandishi habari mjini Tehran.

Urusi ilisema Marekan ina matatizo ya kimfumo ya haki za binadamu, huku vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali nchini China vikiyatazama maandamano hayo katika mche wa mtazamo wa Marekani juu ya maandamano ya kuipinga serikali mjini Hong Kong, ambayo China imesema kwa muda mrefu kwamba Marekani inayahamasisha.

Katika makala ya maoni, gazeti la chama tawala cha kikomunisti la Global Times, lilisema wataalamu wa China wameandika kwamba wanasiasa nchini Marekani wanaweza kutafakari mara mbili kabla ya kuzungumzia tena juu ya Hong Kong, wakijua kwamba maneno yao yanawaza kwenda upogo.

Chanzo: afpe.