1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dunia imeusahau mgogoro wa Kongo kwa ya Ukraine, Gaza - Turk

18 Aprili 2024

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema dunia inasahau vurugu zinazoongezeka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa kulemewa na inayoendelea katika maeneo kama Ukraine na Gaza.

https://p.dw.com/p/4evxi
Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.
Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.Picha: Martal Trezzini/dpa/picture alliance

Turk aliyasema haya wakati wa ziara yake nchini Kongo na kutoa wito wa amani na msaada kwa mamilioni ya watu walioyakimbia makayzi yao.

Baada ya kukutana na watu waliokimbia makaazi yao huko Bulengo karibu na mji mkuu wa eneo hilo, Goma, siku ya Jumatano (Aprili 17), Turk alisema kwamba mgogoro wa kibinadamu lazima uchukuliwe hatua.

Soma zaidi: ADF yashukiwa kuwaua watu 10 mashariki mwa Kongo

"Ni wazi kwamba tunapaswa kuchukua kwa uzito hali hii. Tuna mizozo mingi ulimwenguni, na wakati mwingine nadhani kwamba tunasahau hali ilivyo hapa. Nimekuja hapa ili kuibua hamasa ya ufuatiliaji kutoka kwa jumuiya ya kimataifa juu ya janga linaloendelea hapa." Aliongeza mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Hali ya usalama mashariki mwa Kongo kwa muda mrefu imekuwa ikizidiwa na makundi 120 yenye silaha yananayowania udhibiti wa rasilimali, huku maelfu ya raia wakilazimika kuyahama makaazi yao katika miezi ya hivi karibuni.