1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yatahadharisha ongezeko la homa ya nyani

21 Julai 2024

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kwamba taifa hilo linakabiliwa na "kuongezeka kwa kasi" kwa idadi ya wagonjwa wa Homa ya nyani, Mpox.

https://p.dw.com/p/4iYOs
Dalili ya homa ya nyani
Vipele kwenye ngozi kutokana na maabukizi ya hima ya nyani.Picha: Bihlmayerfotografie/IMAGO

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya hapo jana alisema idadi ya wanaoshukiwa kupata maambukizi imefikia watu 11,166, ikiwa ni pamoja na vifo 450.

Soma pia; Jamhuri ya Kongo yaripoti visa kadhaa vya homa ya nyani, mpox

Muyaya amesema ripoti ya wizara ya afya imefichua ongezeko kubwa la idadi ya visa vya maambukizi, huku mkoa wa magharibi wa Equateur ukiathirika zaidi.

Aidha ripoti hiyo imesema serikali inachukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo, hasa katika huduma ya matibabu, ufuatiliaji wa mawasiliano na maeneo husika ya afya na kuongeza ufuatiliaji miongoni mwa jamii.

Haya yanajiri siku chache baada ya Shirika la Afya Duniani kuonya juu ya tishio la afya duniani linaloletwa na ugonjwa wa huo  "Mpox" huku kukiwa na wasiwasi wa uwezekano wa kutokea mlipuko wa aina mpya ya virusi hatari zaidi nchini Kongo.