1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yamtaja Mmarekani kwa kuhusishwa na jaribio la mapinduzi

22 Mei 2024

Msemaji wa Jeshi la Congo Brigadia Jenerali Sylvain Ekenge, ametangaza jina la Mmarekani wa tatu anaedaiwa kuhusika na jaribio lililoshindwa la kuipindua serikali.

https://p.dw.com/p/4g8jv
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Jaribio la mapinduzi | Ikulu ya Taifa mjini Kinshasa
Mtu aliyeavaa vazi la kijeshi akiongea ndani ya Ikulu ya Taifa wakati wa jaribio la mapinduzi huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 19, 2024.Picha: Christian Malanga/Handout/REUTERS

Tangazo hilo linatolewa katika kipindi hiki ambacho familia ya  Christian Malanga aliyeongoza  tukio hilo, ikiomboleza kifo chake baada ya kuuwawa katika makabiliano ya risasi.

Jenerali Ekenge ameliambia shirika la habari la The Associated Press kwamba Mmarekani huyo wa tatu ni Taylor Thomson. Haijawa wazi iwapo Thomson ni miongoni mwa waliokamatwa au kuuwawa katika tukio hilo lililotokea katika Ikulu ya rais na jengine katika makaazi ya mshirika wa karibu wa  rais wa Congo Felix Tshisekedi.

Siku ya Jumapili Jeshi la Congo lilitangaza kufanikiwa kuzima  jaribio hilo la kuipindua serikali lililowahusisha raia wakigeni pamoja na wakongomani. Umoja wa Afrika kupitia mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya umoja huo Moussa Faki Mahamat, ililani  jaribio hilo na kukosoa pia matumizi yoyote ya nguvu ya kubadilisha utaratibu wa kikatiba katika nchi yoyote ile ya kiafrika.