1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Wito watolewa FARDC na UPDF kuungana kukabili ADF-Nalu

Benjamin Kasembe/DW Goma25 Juni 2020

Wabunge na watetezi wa haki za binadamu eneo la Beni wameitaka serikali ya Kinshasa kufanya mapatano kati ya jeshi la Congo FARDC na la Uganda UPDF katika harakati za kuwasaka waasi wa ADF-NALU ambao hutoka Uganda,

https://p.dw.com/p/3eJVy
Demorkatische Republik Kongo - Soldaten der Democratic Republic of Congo nach Kämpfen mit Rebellen
Picha: Reuters/G. Tomsaevic

Wabunge hao wanaitaka serikali ya Congo kufanya mapatano pamoja na jeshi kutoka nchi jirani ya Uganda kama njia mojawapo ya kuvitokomeza vikundi vya waasi Kivu ya kaskazini, ikiwemo ADF -Nalu wanaopiga kambi katika msitu wa Beni kwa miongo miwili hivi wakiwaua raia kwa shoka na mapanga.

Hata hivyo wabunge hao akiwemo mbunge wa Kivu Kaskazini, katika mazungumzo na DW Kiswahilihii wamedai kuwa kuongezeka kwa mauaji ya raia wilayani Beni kumesababishwa na ukosefu wa mawasiliano kati ya majeshi kutoka mataifa haya mawili ambayo yameshindwa kuafikiana kwak ufanya operesheni za pamoja ili kuwasaka waasi hao wa ADF Nalu.

UN: Watu 13,000 waliuawa DRC miezi minane iliyopita

Hayo ni baada ya Waasi wa ADF wenye asili ya Uganda kufanya shambulizi kali dhidi ya msafara wa askari wa Umoja wa Mataifa wiki hii huko BENI na kumuuwa askari mmoja wa umoja huo na wengine kujeruhiwa. Shambulizi hilo lililaaniwa na wawakilishi wa asasi za kiraia eneo hilo.

Jeshi la Congo (FARDC) limekuwa likijaribu kutokomeza mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi ya wanamgambo katika baadhi ya maeneo ya Congo.
Jeshi la Congo (FARDC) limekuwa likijaribu kutokomeza mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi ya wanamgambo katika baadhi ya maeneo ya Congo. Picha: Reuters/G. Tomsaevic

Wakati huohuo watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa Congo wameunga mkono ombi hilo la wabunge huku wakiitaka serikali kuongeza juhudi za kuwapiga vita waasi hao.

Raia 20 wauawa kaskazini mashariki mwa DRC

Raia hawa wanaoishi katika maeneo hayo yenye vurugu na ambao wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani kutokana na mashambulizi ya waasi dhidi ya vijiji vyao wamekuwa na maoni tofauti baada ya pendekezo hilo la wabunge Kivu ya kaskazini

Waasi wenye asili ya Uganda wameshtumiwa kwa mauwaji ya zaidi ya watu 3.OOO wakiwakata vichwa kwa mapanga na shoka katika eneo hilo la Beni tangu mwaka wa 2014.