1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Mbunge ahukumiwa kifo kwa kosa la uhaini

7 Oktoba 2023

Mahakama ya kijeshi imemhukumu adhabu ya kifo mbunge mmoja nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kosa la uhaini.

https://p.dw.com/p/4XETJ
DR Kongo | Edouard Mwangachuchu
Picha: ZUMA Press/IMAGO

Mbunge huyo ni Edouard Mwangachuchu 70, ambaye anawakilisha eneo la Masisi katika bunge la kitaifa na ambaye anamiliki pia kampuni ya uchimbaji madini.

Jaji mfawidhi Jenerali Robert Kalala amesema Mwangachuchu ambaye hakuwepo wakati ikisomwa hukumu hiyo, alipatikana na hatia ya uhaini, kumiliki silaha kinyume cha sheria na kushiriki katika harakati za uasi wa kundi la M23.

Uamuzi huo umekosolewa vikali na wakili wake aliyesema umechochewa na "chuki ya kikabila". Mahakama imeamuru kuachiwa mara moja kwa mshtakiwa mwenza afisa wa polisi Robert Muchamalirwa.     

Adhabu ya kifo mara nyingi hutolewa nchini Kongo, lakini haijatumika kwa miaka takriban 20 na badala yake hutumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.