DRC kuwarudisha mamilioni ya 'Wanyarwanda'
3 Mei 2013Wito huo umetolewa na waziri wa mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Richard Muyej wakati akiongea na shirika la habari la IPS. Muyeji amesema hayo licha ya kuwa serikaliya Congo inaamini kuwa ni mapema kuchukua hatua hiyo.
Amesema kuwa kwa mujibu wa makubaliaao yalifikiwa kati ya Shirika la Umoja wa mataiafa la kuhudumia wakimbizi UNHCR,Rwanda na Serikali ya Congo,wakimbizi hao wana haki ya kurudishwa kwao kwa hiyari.
Wito huo unatolewa na Serikali ya Congo huku UNHCR ikisisitiza kuwa Juni 30 mwaka huu ndio mwisho wa kuwapo wakimbizi hao na kuwa sheria ya kuwarudisha katika nchi zao,inahitaji wakimbizi wenyewe wachague kurudi kwa hiari,lakini pia wanahaki ya kuomba kubiakia kuwa wakimbizi au kuomba uraia.
Katika mkutano wa wa kimataiafa kuhusu wakimbizi wa Rwanda uliofanyika Brussels kuanzia Aprili 19-20,2013,Serikali ya Congo ililitaka UNHCR na nchi za kanda hiyo kufikiria juu ya hali ya usalama kwa wakimbizi wa Rwanda nchini Congo.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Rwanda National Congress CNR Gervais Condo,chanye makao makuu yake Marekani,ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa Brussels aliliambia shirika la habari la IPS,kuwa hakuna mazingira yanayoonesha kuwa hali ya ukimbizi ni suluhisho la kuchukua muda mrefu.
Makakati wa kuwarudisha wakimbizi una changamoto
“Lakini hatuezi kutegemea wakimbizi kurudi nyumbani kwao bila kujua sababu iliowafanya kuwa wakimbizi''amesema Condo msaidizi wa Jenerali, Kayumba Nyamwasa,kiongozi wa zamani wa jeshi la Rwanda,mwenyekiti na muasisi wa CNR ambaye sasa anaisha uhamishoni Afrika Kusini.
Kwa upande wake serikali ya Rwanda imedokeza kuwa kwa sasa hali ni salama katika nchi za Maziwa makuuu,hivyo hakuna haja ya kusubiri Juni 30 mwaka huu kufanyia kazi kifungu cha sheria ya wakimbizi kililichowekwe katika mkutano wa mwaka 1951mjini Geneva.
Kati ya mwaka 1994 ambapo Chama cha Patriotic Front kilishika madaraka nchini Rwanda kufatia mauaji ya kimbari,na kufikia Februari mwaka huu,Shirika hilo la Umoja wa Mataifa, tayari imeshawarudisha nyumbani jumla ya wakimbizi milioni 3.
Mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo yanakadiriwa kupoteza maisha ya zaidi ya watu milioni moja wengi wao wakiwa kutoka kabila Wachache Watutsi na Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani.
Wakimbizi wa Rwanda waliokimbia nchini mwao kati ya miaka ya1959 na1998,wana hofu kutokana na kutobadilishwa hali ya kutokuwa na uhuru wa kuongeaa na kujumuika na jamii nchini Rwanda. Aliekuwa mwanasheria mkuu Gérard Gahima na balozi wa zamani Théogène Rudasingwa ni miongoni mwa viongozi wanaoishi uhamishoni.
Mwandishi :Hashim Gulana/ IPS
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman