Dikteta wa Guinea ahukumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu
1 Agosti 2024Kiongozi wa kijeshi wa zamani nchini Guinea ya Conakry Moussa Camara amehukumuwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya mahakama ya mjini Conackry kumpata na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Soma pia: Kiongozi wa zamani wa Kijeshi wa Guinea atoroshwa gerezani
Camara alihukumiwa Jumatano kwa mauaji ya watu 157 mnamo mwaka 2009. Wanajeshi waliwaua watu hao katika uwanja wa michezo mjini Conackry ambapo wanawake kadhaa pia walibakwa.
Mahakama ya Jinai nchini humo ilimtia hatiani Camara na maafisa wengine saba wa ngazi ya juu baada ya kusikilizwa kesi hiyo ya mauaji, utekaji nyara na ubakaji iliyochukua muda mrefu. Washtakiwa wanne waliachiliwa huru.
Soma pia:Viongozi wa kiraia waachiwa huru Guinea
Zaidi ya watu 100 walionusurika na jamaa za waathiriwa walitoa ushahidi katika kesi hiyo iliyoanza Novemba mwaka 2022.