1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroDenmark

Denmark kuipa Ukraine ndege za kivita robo ya pili ya mwaka

6 Januari 2024

Denmark imesema itaipatia Ukraine ndege za kwanza 19 za kivita chapa F-16 katika robo ya pili ya mwaka huu baada ya marubani wa Ukraine kukamilisha mafunzo ya kuzirusha.

https://p.dw.com/p/4avgi
Ndege ya kivita chapa F-16
Ndege ya kivita chapa F-16 Picha: Axel Heimken/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na wizara ya ulinzi ya Denmark katika taarifa yake iliyotolewa leo kuhusu mipango ya kuipatia Ukraine ndege hizo mamboleo zinazoundwa nchini Marekani. Denmark ilitangaza mwezi Agosti mwaka jana uamuzi wa kuipatia Ukraine ndege hizo baada ya kupata idhini kutoka kwa Marekani.

Ukraine ilikuwa ikiyashinikiza mataifa ya magharibi kuipatia ndege za kisasa za kivita baada ya kupoteza sehemu kubwa ya ndege zake kwenye vita na Urusi.

Marekani ilijizuia kwa miezi kadhaa kuidhinisha upelekwaji wa ndege inazoziunda nchini Ukraine kwa mashaka kwamba hatua hiyo huenda ingetafsiriwa na Moscow kuwa uchokozi wa moja kwa moja kwenye vita vinavyoendelea .