Dbeibah: Atoa wito wa katiba kupatikana kabla ya uchaguzi
24 Januari 2022Matangazo
Dbeibah amesema katiba inahitajika hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ili kuilinda nchi na raia wa Libya pamoja na kusimamia chaguzi.
Katika mjadala uliofanyika jana mjini Tripoli uliowashirikisha maafisa mbali mbali akiwemo mkuu wa baraza la juu ya serikali, Khaled al Mechri, waziri mkuu Dbeiba aliongeza kusema kwamba walibya wanahitaji uchaguzi huru utakaoheshimu matakwa yao na sio kutanuliwa kwa mgogoro kwa kuwekwa serikali nyingine ya mpito.
Kwa mujibu wa waziri mkuu huyo tatizo kubwa la Linya hivi sasa ni kukosekana katiba.
Spika wa bunge Aguila Saleh analaumiwa kwa kuchangia kuuongeza mgogoro wa Libya kutokana na hatua yake ya kubadili sheria muhimu na kuwapendelea wagombea fulani kuelekea uchaguzi mkuu.