1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

David Lammy kuhudhuria mazungumzo ya Umoja wa Ulaya

14 Oktoba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy ataungana leo na mawaziri wenzake wa EU kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili, huku serikali ya nchi hiyo ikilenga kujenga upya uhusiano na Ulaya.

https://p.dw.com/p/4ljz2
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza - David Lammy akihudhuria warsha ya kampeini huko Wales mnamo Mei 30, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza - David LammyPicha: Maja Smiejkowska/REUTERS

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema kuwa Lammy ataungana na kundi la mawaziri  27 wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya kwa mazungumzo huko Luxembourg kuhusu Mashariki ya Kati na vita nchini Ukraine.

Mualiko wa Lammy unafuatia ziara ya waziri mkuu wa Uingereza Brussels

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja huo wa Ulaya, Josep Borrell, alitoa mwaliko kwa Lammy, ambao ulifuatia ziara ya hivi karibuni ya waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer huko Brussels ambapo alijitolea kujenga uhusiano huo hata baada ya nchi hiyo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

Lammy amesema ziara hiyo ni fursa kwa Uingereza kurejea mezani, kujadili masuala muhimu zaidi ya kimataifa na majirani zao wa karibu na pia kuimarisha uhusiano na washirika wao wa Ulaya ili kuwafanya wote kuwa salama zaidi.