1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dabi ya Madrid yakosa mvuto

30 Septemba 2024

Jumapili kulichezwa mechi ya Madrid dabi katika Ligi Kuu ya Uhispania, La Liga, ambapo Atletico Madrid waliokuwa nyumbani waliishia kutoka sare ya bao moja na Real Madrid.

https://p.dw.com/p/4lFhK
Kiungo wa Real Madrid Federico Valverde
Kiungo wa Real Madrid Federico ValverdePicha: Jennifer Lorenzini/REUTERS

Real Madrid ndio walioingia uongozini kupitia kwa Eder Militao halafu Atletico wakasawazisha katika dakika za jioni kabisa kupitia kwa Angel Correa.

Mechi hiyo ililazimika kusimamishwa na muamuzi katika dakika ya 68 baada ya mashabiki wa Atletico kumrushia vitu mlinda lango wa Real Thibaut Courtois.

Mechi hiyo ilisimamishwa kwa kipindi cha dakika 20 nzima na kocha wa Atletico Diego Simeone sasa anasema ni sharti hatua zichukuliwe kuwaadhibu mashabiki wanaoharibu mchezo kwa vitendo kama hivyo ila pia wachezaji wanaochochoea mambo kama hayo, akimlenga mlinda lango wa Madrid Courtois ambaye alimtuhumu kwa kuwachochea mashabiki kumshambulia.

"Lakini pia tuwe makini kwa kile tzunachowafanyia wahanga na najijumuisha mwenyewe hapa. Tuchukue jukumu kwa kila kitu na kwa watu wanaotazama. Imeonekana wazi kabisa Courtois alipokuwa akiwacheka mashabiki na hilo ndilo lililosababisha yaliyotokea," alisema Simeone.

Madrid walimkosa mshambuliaji wao wa kutegemewa katika mechi hiyo Kylian Mbappe ambaye ana jeraha.

Chanzo: Reuters/AP