1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Freddy chatarajiwa kupungua kasi Msumbuji, Malawi

15 Machi 2023

Kimbunga Freddy ambacho kilizipiga Msumbuji na Malawi tangu wiki iliyopita kinatarajiwa kupunguza kasi yake na kuhama kutoka nchi kavu, ikiwa ni ahueni kwa maeneo yaliyoharibiwa na mvua kubwa na upepo mkali.

https://p.dw.com/p/4OhWk
Malawi Mosambik Zyklon Tropensturm Freddy
Picha: Thoko Chikondi/AP Photo/picture alliance

 

Kimbunga hicho kimewauwa karibu watu 200 katika mkoa wa kaskazini mwa Malawi na maeneo ya ndani na karibu na kitovu cha kibiashara nchini humo, Blantyre.

Katika nchi jirani Msumbuji, maafisa wamesema karibu watu 20 walikufa tangu kimbunga hicho kilipotua katika nchi kavu katika mji wa bandari wa Quelimane Jumamosi usiku.

Soma pia:Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga Freddy yapindukia 100

Maafisa nchini Malawi wamesema kuna idadi kubwa ya waliojeruhiwa, wasiojulikana waliko, au kufa na idadi hiyo itaongezeka katika siku chache zijazo.

Malawi ambayo imekuwaikipambana na mripuko wa kipindupindu kabla ya kimbunga hicho, ipo katika hatari ya kurejea kwa ugonjwa huo.