CPJ yamtaka Magufuli amuwachie Kabendera
13 Agosti 2019Shirika hilo la kimataifa lilitaka pia kupatiwa maelezo ya kina kuhusu hatima ya mwandishi wa habari ambaye hajulikani aliko, Azory Gwanda.
Katika barua hiyo ya wazi, shirika hilo linaalowalinda waandishi habari limekumbusha ahadi zilizotolewa mwezi uliopita na Waziri wa Nje wa Tanzania, Palamagamba Kabudi, mjini London alipothibitisha serikali yake inataka "kuwezesha uandishi wa habari waa kiuchunguzi na kuhakikisha waandishi wa habari wanalindwa dhidi ya hatua za kushitakiwa au kukamatwa."
Kabendera alichukuliwa kwa nguvu nyumbanai kwake Julai 29 na tangu wakati huo hoja mpya zimekuwa zikitolewa kuhusu sababu za kushikiliwa kwake.
Tayari serikali ya Tanzania imemfungulia mashitaka ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi, miongoni mwa mengine, ambayo kimsingi hayana dhamana kwenye taifa hilo la mashariki ya Afrika.
Kwa upande wake, Gwanda ambae pia ni mwandishi habari wa kujitegemea hajulikani aliko tangu Novemba 21, 2017.