CPJ yaitaka Pakistan ichunguze mauaji ya mwandishi wa habari
23 Machi 2024Wito wa shirika hilo unatolewa katika wakati huu ambapo kunashuhudiwa mashambulizi dhidi ya waandishi na vyombo vya habari.
Mapema mwezi huu mwandishi wa gazeti la kila siku la Daily Khabrain Jam Saghir Ahmed Lar, aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Punjab.
Mratibu wa CPJ kanda ya Asia, Beh Lih Yi amesema kwamba serikali ya Pakistan lazima iongeze ulinzi kwa vyombo vya habari na kuhakikisha wanahabari wanafanya kazi yao bila kuhofia kulipiziwa kisasi.
Soma pia:CPJ: Waandishi 99 waliuawa kufuatiamzozo wa Israel-Hamas
Malalamiko ya mashambulizi, vitisho na unyanyasaji mtandaoni dhidi ya waandishi wa habari wanaokosoa jeshi, yamekuwa ya kawaida nchini Pakistan.
Kwa mujibu wa CPJ tangu 1992 waandishi wa habari 64 wameuwawa kwa kuhusishwa na kazi zao nchini Pakistan.