1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COVID-19: Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania

George Njogopa22 Januari 2021

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwapiga marukufu abiria wote kutoka Tanzania ili kuepusha kusambaa kwa COVID-19. Hii ni licha ya Tanzania kushikilia kuwa hakuna ugonjwa huo nchini humo.

https://p.dw.com/p/3oGwt
Tansania | Julius Nyerere International Airport - Passagiere werden auf Corona Virus überprüft
Picha: Tanzania Airport Authorities/B. Mollel

Licha ya Serikali ya Tanzania kuendelea kusisitiza imeshinda katika mapambano ya janga la virusi vya corona na kudai kuwa hakuna hata mgonjwa yeyote mwenye maambukizi ya COVID-19, 

Marufuku hiyo ya Uingereza imechukuliwa kama hatua ya kudhibiti aina mpya ya maambukizi ya virusi vya corona vilivyogundulika hivi karibuni nchini Afrika Kusini. Waziri wa Usafirishaji wa Uingereza, Grant Shapps katika taarifa aliyoitoa kupitia akaunti yake ya Twitter anasema kwamba, abiria kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hawaruhusiwi kuingia Uingereza na Ireland.

Soma pia: TCRA yawaonya raia kutosambaza taarifa za COVID-19

Marufuku hiyo inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi na inakusudiwa kudumu kwa takriban wiki mbili. Uingereza inakuwa nchi ya kwanza ndani ya mataifa ya bara ya Ulaya kuitaja moja kwa moja Tanzania kama abiria wake hawaruhusiwi kuingia nchini humo tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona Desemba 2019.

Waziri wa Usafiri wa Uingereza, Grant Shapps katika taarifa aliyoitoa kupitia akaunti yake ya Twitter anasema kwamba, abiria kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hawaruhusiwi kuingia Uingereza na Ireland.
Waziri wa Usafiri wa Uingereza, Grant Shapps katika taarifa aliyoitoa kupitia akaunti yake ya Twitter anasema kwamba, abiria kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hawaruhusiwi kuingia Uingereza na Ireland.Picha: Jeff J Mitchell/Getty Images

Kwa wakati fulani mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na yale ya Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC yamewahi kuingia katika mvutano na Tanzania baada ya kutofautiana namna ya kulishughulikia janga hili la corona. Mataifa hayo yaliwapiga marufuku madereva wa Tanzania kuingia katika nchini zao.

Soma pia: Chanjo zaanza kutolewa katika Umoja wa Ulaya

Wakati huu ambako Uingereza imepiga marufuku abiria wa Tanzania, ingawa kumekuwa na ripoti zisizo rasmi zinazodai baadhi ya watu kujihisi kama vile wanakumbana na dalili zinazofanana na homa hiyo, hata hivyo karibu asilimia kubwa ya wananchi wanaendelea na maisha yao kama kawaida.

Wengi wanasema hawana wasiwasi kuhusu kuwepo ugonjwa huo na wanaendelea na maisha yao bila wasiwasi wowote.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikishikilia kuwa virusi hivyo havipo nchini humo.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikishikilia kuwa virusi hivyo havipo nchini humo.Picha: picture-alliance/M. Schönherr

Wakati mataifa mengine yakipambana na janga hili ikiwamo mataifa yaliyoko jirani, Rais wa Tanzania John Magufuli alisema mwaka jana kuwa taifa hili liko huru na maambukizi ya virusi vya corona na akitoa shukrani kwa Mungu kwa kujibu maombi.

Serikali ya Tanzania imeondoa marufuku ya wageni wanaoingia nchini kukaa karantini kwa muda wa siku 14, pamoja na kuwataka wageni kuonesha vyeti vya vipimo vya COVID-19 vinavyowaonesha kuwa hawana maambukizi. Hata hivyo, hivi karibuni serikali hiyo ilitangaza mwongozo mpya kuhusiana na vipimo vya ugonjwa huo huku ikiongeza gharama za upimaji.