Condolleza Rice ziarani Colombia
26 Januari 2008Matangazo
MEDELIN:
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani-Condoleeza Rice amekutana kwa mazungumzo na rais wa Colombia-Alvaro Uribe,baada ya kukamilisha shughuli ya kukuza mkataba wa soko huru nchini humo.Rais Uribe ameuelezea mkataba huo kama hatua muhimu ya kuwekeza zaidi nchini Colombia.Lakini baraza la Congress ambalo linadhibitiwa na chama cha Democrat limekataa kukubali mkataba huo.Yeye rais wa Venezuela-Hugo Chaves- anasema Marekani na Colombia wanapanga kile alichokiita uvamizi wa kijeshi dhidi ya nchi yake,ingawa hakutoa ushahidi.Kiongozi wa Venezuela amesema kuwa hiyo ndio sababu maalum ya zaira ya Rice nchini Colombia aliyoiita makucha ya ufalme wa Amerika ya Kaskazini.